Mkude ameyasema hayo akiwa kambini muda chache kabla ya mchezo wa leo ambao utapigwa saa 11 jioni katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Mkude amewaambia nyota wenzie kuwa historia ya mechi za Simba na Yanga hudumu muda mrefu kwa vizazi na vizazi hivyo haitapendeza wao kuacha historia kuwa ndiyo kikosi kilichofungwa mara nyingi zaidi na mtani.
Advertisement
“Imetosha sasa kufungwa na hao, mechi ya leo twendeni tukalinde heshima yetu na heshima ya klabu haiwezekani tufungwe sisi kila siku,” amesema Mkude.