Simba Sports Club
News

Mkude asimulia bao lake dhidi ya Prisons Sokoine

14 Sep 2022

Mkude alifunga bao hilo dakika ya 86 akiwa ndani ya 18 akimalizia pasi ya kichwa iliyopigwa na Kibu Denis kufuatia mpira wa adhabu wa Shomari Kapombe.

Mkude ambaye amekosa mechi mbili kutokana na kuwa majeruhi amesema mchezo ulikuwa mgumu tulipata nafasi tukashindwa kuzitumia kama ilivyokuwa kwa Prisons lakini Mungu amekuwa upande wetu na kufanikisha kupatikana kwa alama tatu.

Amesema licha ya kutokea kuuguza majeraha, Mkude amesema alikuwa na kiu ya kuona timu ikishinda katika Uwanja wa Sokoine bila kujali nani atafunga mabao hayo kutokana na kuwa na historia ya kufungwa katika uwanja huo.

Advertisement

"Mchezo ulikuwa mgumu, tulipata nafasi nyingi lakini hatukufunga dakika za mwisho nimefunga na kuisaidia timu kupata ushindi muhimu na hilo ni jambo la kumshukuru Mungu.

"Kiu yangu ilikuwa kuona timu inashinda Sokoine kutokana na historia wengi mnajua, lakini imetokea bahati hiyo imeniangukia momi namshukuru Mungu, benchi la ufundi na timu kwa ujumla. Kikubwa mashabiki wetu ,wasiogope hwaendelee kutisapoti huu ni mwanzo tu mazuri yanakuja msimu huu," amesema Mkude.

Bao hili ni la kwanza kwa Mkude msimu huu baada ya kucheza mechi mbili baada ya kukosa nyingine mbili kutokana na kuwa majeruhi.

Back to homepage
Share this story