Kiungo wetu mkabaji Jonas Mkude, amekabidhiwa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki wa Mwezi Desemba (Emirate Aluminium Simba Fans Player of the Month).
Mkude ameonyesha kiwango safi ndani ya mwezi Desemba akiwashinda walinzi wa kati Joash Onyango na Henock Inonga.
Baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Mkude amewashukuru wachezaji wenzake, benchi la ufundi na mashabiki waliompigia kura akashinda.
Mkude ameongeza kuwa tuzo hiyo imemuongezea morali na kuendelea kujituma kwa ajili ya kuisaidia timu kufanya vizuri na kuwapa mashabiki furaha.
"Kila mchezaji anajitahidi kufanya vizuri kuisaidia timu na kuwafurahisha mashabiki, mimi ni mmoja wao. Nawashukuru wachezaji wenzangu kwa msaada maana bila wao nisingeweza. Pia nalishukuru benchi la ufundi kunipa nafasi na mashabiki kunipigia kura," amesema Mkude.
Mkude amekabidhiwa tuzo na fedha taslimu Sh 2,000,000 kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminum ACP kama sehemu ya zawadi.