Igendia (36) anachukua nafasi ya Patrick Rweyemamu ambaye amekuwa Mkuu wa Programu za soka la vijana.
Ujio wa Igendia unaongeza ufanisi katika benchi la ufundi kwakuwa yupo vizuri pia kwenye utimamu wa mwili pamoja na utawala wa timu.
Advertisement
Igendia amewahi kufanya kazi na Gormahia FC, timu ya Taifa ya Kenya 'Harambee Stars' pamoja na timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'.
Uwepo Igendia kwenye kikosi ni sehemu ya kuliboresha benchi letu la ufundi kuelekea msimu mpya wa Ligi 2023/24.