Magori amesema siku zote rangi nyekundu ni rangi ya Mamlaka na lengo la Uongozi ni kuzidi kuifanya kuwa klabu bora zaidi ndani na nje ya nchi.
“Mwaka huu Simba inakwenda kutimiza miaka 90, tutafanya mambo makubwa, Rangi nyekundu ni rangi ya Mamlaka, Mimi, Murtaza Mangungu na Bodi nzima tuko imara na tumeshaanza kufanya usajili wa dirisha kubwa. Hii sio timu ya maneno maneno, kama unataka mpira njoo Simba," amesema Magori.
Kuhusu ujenzi wa Uwanja wetu tutakaotumia kwenye mechi zetu, Magori amesema tayari amejulishwa kuwa muwekezaji ameomba kujenga kwenye eneo letu la Bunju na mchakato unaendelea.
“Nimejulishwa na Wadhamini wa Klabu kwamba mwekezaji ameomba kujenga uwanja kwenye eneo letu la Bunju, Mdhamini mmoja alinipigia akaniambia litakuja kwenye bodi tulichakate."
"JayRutty ni mzabuni wa Simba wa vifaa vya michezo, kila mwaka anatoa bilioni tano za ujenzi wa uwanja. Tutakaa nae tuone mipango yake kwahiyo labda badala ya kujenga uwanja wa watu 8,000 hiyo Bilioni tano tutatumia kuboresha sehemu nyingine," amesema Magori.
Kuhusu mabadiliko ya Katiba mpaka sasa Magori amesema “Kuna mabadiliko ya katiba ambayo yanafanyika kati ya wadhamini wa klabu na mwekezaji. Kamati inaendelea na kazi ili kurekebisha kule BRELA na mambo mengine yataendelea.