Winga Yusuf Mhilu amesema ushindi katika mchezo wa Jumatano dhidi ya Kagera Sugar utaturudisha kwenye ramani ya kupigania ubingwa wetu msimu huu.
Mhilu amesema baada ya kutopata ushindi katika mechi zetu mbili za ligi zilizopita wachezaji na benchi la ufundi wanafahamu alama tatu zitatufanya kurudi katika mstari.
Nyota huyo wa zamani wa Kagera ameongeza kuwa mchezo utakuwa mgumu kwa kuwa wapinzani nao wanataka kushinda ili kujiondoa kwenye nafasi mbaya waliyopo katika msimamo.
"Mchezo utakuwa mgumu kutokana na Kagera nao wanahitaji kujinasua katika nafasi waliyopo, nasi tunataka ushindi ili kurudi kwenye ramani ya kutafuta ubingwa.
"Benchi la ufundi pamoja na wachezaji tunajua umuhimu wa mchezo huo na tumejipanga kuhakikisha tunashinda ili pia kuwapa furaha mashabiki wetu," amesema Mhilu.