Mhilu alifunga bao hilo jana dakika ya 52 kabla ya kuongeza jingine dakika ya 88 katika ushindi wa mabao 4-0 tuliopata dhidi ya Pamba FC katika mchezo wa Robo Fainali ya Azam Sports Federation Cup.
Mhilu amesema ni furaha kwa kila mchezaji kufunga na kuisaidia timu kupata ushindi ambapo alikuwa anaisubiri kwa hamu siku ya jana ifike.
"Nimefurahi sana kufunga bao la kwanza nikiwa na jezi ya Simba. Ni ndoto ya kila mchezaji kufunga na kuisaidia timu kupata ushindi.
"Nawashukuru wachezaji wenzangu kwa kunipa ushirikiano mkubwa pamoja na benchi la ufundi kuniamini na kunipa nafasi naamini nitaendelea kufanya vizuri kuisaidia timu," amesema Mhilu.
Mhilu amewaomba mashabiki kuendelea kujitokeza kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu kwa kuwa bado msimu haujaisha na mapambano yanaendelea.