Simba Sports Club
News

Mgunda: Tupo Tayari kwa mchezo dhidi ya Dodoma Jiji

16 May 2024

Mgunda amesema kikosi kipo kwenye hali nzuri na kimepata siku mbili za kufanya mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa kesho ambao tunategemea utakuwa mgumu kutokana na nafasi waliopo Dodoma.

Mgunda ameongeza kuwa kiungo mshambuliaji Saido Ntibazonkiza aliyekuwa majeruhi amejiunga na kikosi pamoja na Fabrice Ngoma aliyekuwa anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano nae akiwa amerejea.

Kwa upande wa Clatous Chama na Luis Miquissone wao wamefanya mazoezi pamoja na wenzao na afya zao zimetengemaa lakini bado hawako tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho.

Advertisement

"Maandalizi ya mchezo ya kucheza na timu bora yamekamilika, tunaamini utakuwa mgumu lakini tupo tayari," amesema Mgunda.

Kwa upande wake nahodha msaidizi Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' amesema wao kama wachezaji wapo tayari kupambana hadi mwisho ili kuiwezesha timu kupata matokeo chanya.

"Tumekuja kamili kwa ajili ya kupambana na Dodoma ili tupate pointi zote tatu," amesema Zimbwe Jr

Back to homepage
Share this story