Simba Sports Club
News

Mgunda: Tunarudi kumalizia kwa Mkapa

9 Oct 2022

Mgunda amesema mchezo wa marudiano hautakuwa rahisi licha ya mtaji mzuri wa mabao na hatutawadharau Premiero De Agosto badala yake tutajipanga kuhakikisha tunashinda.

Mgunda ameongeza kuwa kwa sasa bado mshikamano kwa Wanasimba unahitajika ili kutimiza malengo yetu tuliyojiwekea kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Advertisement

"Tunamshukuru Mungu tumepata ushindi mnono ugenini lakini hii haimaniishi tumemaliza kazi hapana. Hii ni mechi ya kwanza kuna nyingine tutacheza nyumbani.

"De Agosto sio timu mbaya ni mabingwa wa Angola pamoja na ushindi wa leo lakini bado hatujafuzu, tunarudi nyumbani kujipanga kwa ajili ya mchezo wa marudiano," amesema Mgunda.

Back to homepage
Share this story