Mgunda amesema mchezo mmoja unapoisha maandalizi ya unaofuata yanaanzia pale pale kwahiyo kwa sasa mipango yetu ni kufanya vizuri katika mechi zilizobaki.
Akizungumzia mchezo dhidi ya Kagera, Mgunda amesema ulikuwa mgumu lakini tuliweza kutengeneza nafasi nyingi ingawa hatukuweza kuzitumia.
Mgunda amekataa kuwalaumu wachezaji moja kwa moja kutokana na kupoteza nafasi zilizo tengenezwa badala yake amesema kwenye mpira ni kawaida kutokea.
Advertisement
"Tumetengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini hatukuweza kuzitumia na hilo sio jambo jipya kwenye soka, ni kawaida na huwa inatokea."
"Mechi ya Kagera imemalizika sasa tunajiandaa kwa mechi zetu nne zilizosalia kabla ya kumalizika msimu na malengo yetu ni kufanya vizuri," amesema Mgunda.