Simba Sports Club
News

Mgunda: Tunaelekeza nguvu zetu Angola

3 Oct 2022

Kauli hiyo imetolewa na kocha mkuu, Juma Mgunda ambapo amesema maandalizi dhidi ya De Agosto yameanza mara moja kabla ya kikosi kupaa kuelekea Angola.

Mgunda ameongeza kuwa mapungufu yaliyoonekana kwenye mchezo wa jana yatafanyiwa kazi mazoezini kabla ya kukutana na De Agosto mwishoni mwa juma lijalo.

Advertisement

"Tunamshukuru Mungu tumepata ushindi mnono kabla ya mchezo wetu wa Ligi ya Mabingwa, utatuongezea morali katika mechi yetu ya ugenini nchini Angola.

"Maandalizi ya mchezo huo tayari yameanza na kitu kizuri hatutakuwa na mchezo wa ligi hivyo tutapata muda wa kufanya marekebisho yaliyojitokeza mazoezini," amesema Mgunda.

Back to homepage
Share this story