Simba Sports Club
News

Mgunda: Tuliwasoma vizuri Big Bullets

18 Sep 2022

Mgunda amesema baada ya ushindi wa mabao 2-0 ugenini tulijua Bullets watakuja kushambulia kuanzia mwanzo kwa kuwa watakuwa hawana cha kupoteza ndiyo maana na sisi tulijipanga kwa hilo.

Mgunda amesema pamoja na ushindi tuliopata ugenini tulijua bado mechi haikuisha na tulihitaji kupata mabao zaidi ili kujihakikishia kusonga mbele.

Advertisement

"Kama nilivyosema wiki iliyopita mechi ilikuwa haijaisha. Tulijua Big Bullets watakuja kutushambulia kwa kuwa hawana cha kupoteza hivyo tulijiandaa kuwadhibiti na kuhakikisha tunatumia nafasi tunazopata.

"Nawapongeza wachezaji kwa kufuata maelekezo tuliyowapa, wamepambana mpaka mwisho kuwapa furaha Wanasimba," amesema Mgunda.

Back to homepage
Share this story