Simba Sports Club
News

Mgunda: Tuko tayari kwa Prisons kesho

29 Dec 2022

Mgunda amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri na ukiwatoa wale ambao ni majeruhi wa muda mrefu lakini wengine wote wapo tayari kwa mchezo.

Amesema mchezo utakuwa mgumu Prisons ni timu nzuri na tutaingia uwanjani tukiwa tunajua tutapata upinzani mkubwa lakini tumejiandaa kikamilifu kuhakikisha tunapata pointi zote tatu.

"Maandalizi yote ya mchezo yamekamilika wachezaji wapo kwenye hali nzuri, tunategemea kupata upinzani mkubwa lakini tupo tayari kupambana," amesema Mgunda.

Advertisement

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji, mlinzi wa kushoto Gadiel Michael amesema kila kitu sawa kwa upande wao na yeyote atayepata nafasi atakuwa tayari kuitumikia timu.

"Sisi wachezaji tupo tayari kwa mchezo, morali zipo juu. Tunawaheshimu Prisons ni timu nzuri lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata pointi zote," amesema Gadiel.

Back to homepage
Share this story