Simba Sports Club
News

Mgunda: Prisons walitupa upinzani mkubwa

14 Sep 2022

Mgunda amesema mara zote Prisons imekuwa ikitusumbua hasa katika uwanja wao wa nyumbani lakini wachezaji wetu walipambana hadi dakika ya mwisho kupata ushindi.

Mgunda ameongeza kuwa imekuwa jambo zuri kuvunja mwiko na kupata alama tatu muhimu katika Uwanja wa Sokoine ambazo zitaongeza morali kuelekea mechi zilizo mbele yetu.

Advertisement

"Ilikuwa mechi ngumu, wachezaji wangu walipambana mwanzo mpaka mwisho. Tumekuwa tukipata wakati mgumu tukikutana na Prisons hapa Sokoine lakini jambo jema tumepata ushindi.

"Tunamshukuru Mungu tumepata ushindi katika mchezo mgumu, hii itaongeza morali kuelekea mechi zetu zijazo," amesema Mgunda.

Back to homepage
Share this story