Simba Sports Club
News

Mgunda: Mpira ni mchezo wa makosa, Geita sio timu mbovu

18 Dec 2022

Mgunda amesema mpira ni mchezo wa makosa ambapo wenzetu waliyofanya nasi tukayatumia vizuri kupata ushindi mnono.

Mgunda ameongeza kuwa tangu tunatoka Dar es Salaam kuja Mwanza tulikuwa tunajua tunaenda kukutana na timu imara na tulijipanga kuwakabili.

Advertisement

"Kupata ushindi mabao matano haimaanishi Geita ni timu mbovu, bali mpira ni mchezo wa makosa wameyafanya tumeyatumia vizuri.

"Jambo jema tumepata alama tatu ugenini tunajipanga kwa mchezo ujao wa ligi dhidi ya Kagera Sugar," amesema Mgunda.

Back to homepage
Share this story