Kocha Mgunda ametuwezesha kushinda mechi nne na kutoka sare moja katika mwezi huo huku akiwapiku Nasreddine Al Nabi wa Yanga na Hans Van Pluijm wa Singida Big Stars.
Kwa upande wake Chama amekuwa kwenye ubora na takwimu nzuri katika mwezi Desemba akicheza mechi tano sawa na dakika 450 akifunga mabao mawili na asisti tano.
Chama amewapiku Nahodha John Bocco na mshambuliaji Fiston Mayele ambao ameingia nao fainali ya kinyang'anyiro hicho.
Takwimu za Mgunda za Desemba
Coastal Union 0-3 Simba
Advertisement
Geita Gold 0-5 Simba
Kagera Sugar 1-1 Simba
KMC 1-3 Simba
Simba 7-1 Tanzania Prisons
Mgunda ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya pili mfululizo baada ya kufanya hivyo pia mwezi Novemba.