Simba Sports Club
News

Mgunda awapongeza wachezaji ushindi wa Prisons

30 Dec 2022

Mgunda amesema wachezaji wamejitahidi kufuata maelekezo hasa kipindi cha pili na ndicho kilichotusaidia kupata ushindi huo mnono wa kufungia mwaka 2022.

Akizungumzia kiwango cha nyota mpya Said Ntibazonkiza, Mgunda amesema ni mchezaji mzuri na uzoefu wake utasaidia katika kikosi.

Advertisement

"Baada ya mlinzi Henock Inonga kuumia wachezaji wenzake waliingia unyonge wakawa hawako vizuri, kipindi cha pili tuliwajenga kisaikolojia na walivyorudi wakafanya vizuri nawashukuru kwa kufuata maelekezo kwa usahihi na kutupatia ushindi mnono.

"Ntibazonkiza ni mchezaji mzuri tunaamini uzoefu wake utatusaidia na ndiyo maana tukamsajili," amesema Mgunda.

Back to homepage
Share this story