Simba Sports Club
News

Mgunda akabidhiwa tuzo yake CCM Kirumba

18 Dec 2022

Mgunda amewashinda makocha Hans Van Pluijm wa Singida Big Stars na Meck Mexime wa Kagera Sugar ambao aliingia nao fainali ya kinyang'anyiro hicho.

Katika mwezi Novemba Mgunda ametuwezesha kushinda mechi nne dhidi ya Ihefu, Namungo, Ruvu Shooting na Polisi Tanzania na tukitoka sare dhidi ya Mbeya City na Singida Big Stars.

Advertisement

Hii ni mara ya kwanza kwa Mgunda kushindika tuzo ya kocha bora wa mwezi tangu ajiunge na kikosi chetu Septemba mwaka huu.

Mgunda amekabidhiwa tuzo hiyo na Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Steven Mguto huku akipokea mfano wa hundi ya Sh. 1,000,000.

Back to homepage
Share this story