Simba Sports Club
News

Mgunda afanya mabadiliko mawili dhidi ya Ihefu leo

12 Nov 2022 By simbasc 343 views
Kocha Juma Mgunda, amefanya mabadiliko ya wachezaji wawili katika mchezo wa leo dhidi ya Ihefu FC utakaopigiwa saa moja usiku kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa. Katika mchezo uliopita dhidi ya Singida Big Stars, Mgunda aliwapanga viungo watatu kwenye eneo la ulinzi lakini leo kawaanzisha wawili Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin. Habib Kyombo ambaye alitokea benchi katika mchezo uliopita leo ataongoza safu ya ushambuliaji pamoja na Moses Phiri. Augustine Okrah ambaye mchezo uliopita hakucheza ameanza akichukua nafasi ya Kibu Denis ambaye yupo benchi. Kikosi kamili kilivyopangwa Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Sadio Kanoute (13), Pape Sakho (10), Mzamiru Yassin (19), Habibu Kyombo (32), Moses Phiri (25), Augustine Okrah (27). Wachezaji wa Akiba Beno Kakolanya (30), Erasto Nyoni (18), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Mohamed Ouattara (33), Victor Akpan (6), Nassor Kapama (35), Kibu Denis (38).
Advertisement
Back to homepage
Share this story