Simba Sports Club
News

Mgunda afanya mabadiliko matatu dhidi ya Singida leo

9 Nov 2022 By simbasc 390 views
Kocha Mkuu Juma Mgunda, amefanya mabadiliko ya wachezaji watatu kuelekea mchezo wetu wa leo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Big Stars utakaopigwa Uwanja wa Liti saa 10 jioni. Mgunda amemuanzisha mlinda mlango Beno Kakolanya, kiungo mkabaji Sadio Kanoute na Kibu Denis ambao hawakuanza katika mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar. Moses Phiri ataendelea kuongoza safu ya ushambuliaji ambapo atasaidiwa na Kibu pamoja na Pape Sakho. Kikosi kamili kilivyopangwa Beno Kakolanya (30), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Jonas Mkude (20), Pape Sakho (10), Sadio Kanoute (13), Kibu Denis (38), Moses Phiri (25), Mzamiru Yassin (19). Wachezaji wa Akiba Aishi Manula (28), Erasto Nyoni (18), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Mohamed Ouattara (33), Victor Akpan (6), Peter Banda (11), Nassor Kapama (35), Habibu Kyombo (32).
Advertisement
Back to homepage
Share this story