Simba Sports Club
News

Mgosi: Tupo tayari kutetea Ngao ya Jamii

1 Oct 2024

Mgosi amesema Yanga Princess wamefanya usajili mzuri na wanatamani kuwa kama Simba na hawahitaji kuwa kama wapinzani wetu kwa sababu tupo mbali tumecheza mechi nyingi za kiushindani.

Mgosi amesema hayo katika mkutano wa waandishi wa habari kuelekea mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga Princess utakaochezwa kesho uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge Dar es Salaam.

Advertisement

“Tumefanya maandalizi mazuri, tuko vizuri lakini tutacheza kwa tahadhari kubwa kwa sababu Yanga Princess wamefanya usajili mzuri na wamemrejesha kocha Edna Lema ambaye ni mzoefu wa soka la Wanawake,” amesema Mgosi.

Kwa niaba ya wachezaji mlinzi Fatma Issa 'Fetty Densa' amesema wamejipanga vizuri kazi imebaki kwa wachezaji na hawatawaangusha mashabiki wao kupambana kutetea taji hilo.

Back to homepage
Share this story