Simba Sports Club
News

Mels Daalder Skauti Mkuu Simba.

25 May 2023

Mels ameshiriki kozi mbalimbali za duniani ikiwa ni pamoja na zilizoendeshwa na skauti wa zamani wa Manchester United, David Hobson.

Mels ambaye ameshawahi kuishi Tanzania ni shabiki mkubwa wa Simba pia ni mjuzi wa kufanya upembuzi (analysis) na anaijua vizuri ligi ya Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

Mels anaongea lugha kadhaa ikiwemo Kiholanzi, Kiingereza, Kijerumani, Kifaransa na Kiswahili kwa kiasi fulani.

Advertisement

Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu, Imani Kajula amesema eneo la skauti ni muhimu ingawa lilikuwa haipewi nafasi kubwa na kwa kuliona hilo tumeamua kumleta Mels.

" Tunafuraha kubwa kumkaribisha Mels ili kuja kuboresha ufanisi kwenye skauti kwakuwa ni eneo muhimu katika mafanikio ya klabu yetu. Tunaendelea na maboresho muhimu kuelekea msimu mpya wa ligi na mashindano ya kimataifa," amesema Kajula.

Back to homepage
Share this story