Simba Sports Club
News

Mechi yetu dhidi ya Kagera imeahirishwa

18 Dec 2021

Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar ambao ulipangwa kuchezwa leo katika Uwanja wa Kaitaba umeahirishwa kutokana na wachezaji wetu kuumwa.

Jana Kocha Msaidizi Seleman Matola, aliweka wazi mbele ya waandishi wa habari kuwa robo tatu ya wachezaji wanaumwa kifua, mafua na homa na hali zao bado hazijatengamaa.

Advertisement

Kamishna wa mchezo Nasib Mabruk, amethibitisha kuahirishwa kwa mchezo huo kutokana na kujiridhisha idadi ya wachezaji wanaoumwa ni wengi hivyo mechi haitaweza kuchezwa.

Ugonjwa wa kifua, mafua na homa umeingia kwa kasi nchini huku taarifa zikisema ni mabadiliko ya hali ya hewa.

Back to homepage
Share this story