Simba Sports Club
News

Mechi yetu dhidi ya Ihefu kupigwa kesho saa moja usiku Chamazi

6 Apr 2023

Awali mchezo huo ulipangwa na kutangazwa kuwa utafanyika saa 10 jioni katika dimba hilo hilo la Azam Complex lakini muda huo umebadilishwa sasa utapigwa usiku.

Maamuzi ya kusogeza muda mbele ni kuwapa nafasi mashabiki waliopo kwenye Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kufuturu na wale Wakristo kufanya ibada ya Ijumaa Kuu.

Advertisement

Mchezo huo utakuwa ni wa kwanza kwetu kucheza katika Uwanja wa Azam Complex msimu huu kufuatia ukarabati unaoendelea katika Uwanja wa Benjamin Mkapa tunaotumia kwa mechi za nyumbani.

Back to homepage
Share this story