Sababu ya kuahirishwa kwa mchezo huo ni kutupa nafasi ya kusafiri hadi nchini Ivory Coast kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas utakaopigwa Ijumaa, Februari 23.
Bodi ya Ligi imeona kama tungecheza mchezo dhidi ya Mtibwa tusingepata muda wa kujiandaa na mechi ya ASEC huku ikizingatiwa tunapaswa kusafiri umbali mrefu.
Advertisement
Mchezo wetu ulioahirishwa dhidi ya Mtibwa utapangiwa tarehe nyingine ya kuchezwa.