Mchezo huo ulikuwa haupangiwa tarehe kutokana na ratiba ya ushiriki wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na mechi za kufuzu michuano ya Afrika (AFCON).
Baada ya mchezo wetu wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos ya Zambia utakaopigwa Septemba 16 kikosi kitarejea jijini Dar es Salaam kujiandaa na mechi ya Coastal.
Advertisement
Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) imeweka wazi kuwa mchezo wetu dhidi ya Tanzania Prisons ambao ulipangwa kupigwa Oktoba 3, katika Uwanja wa Sokoine umesogezwa mbele hadi Oktoba 5, kwakuwa mechi yetu ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos itachezwa Oktoba Mosi.