Mchezo huo ulisogezwa mbele kipindi ambacho tulikuwa tunashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ili kutupa nafasi ya maandalizi mazuri.
Baada ya kusogezwa mbele ulikuwa haujapangiwa tarehe ya kuchezwa lakini leo Bodi ya Ligi imeweka hadharani kila kitu.
Advertisement
Pia mchezo wetu wa mwisho wa kufungia msimu wa Ligi Kuu ya NBC 2022/23 dhidi ya Coastal Union utapigwa Mei 28 katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Kikosi kinaendelea na mazoezi chini ya kocha mkuu Roberto Oliviera 'Robertinho' na wasaidizi wake.