Awali CAF iliweka wazi kuwa mechi yetu ingechezwa kati ya tarehe 21 mpaka 23 na sasa itachezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumapili ya Novemba, 23 saa 10 jioni.
Tayari kikosi chetu kinaendelea na maandalizi ya mchezo huo muhimu ambao malengo yetu ni kuhakikisha tunapata ushindi nyumbani.
Advertisement
Leo asubuhi kikosi kimecheza mechi ya kirafiki ya kimazoezi iliyopigwa Uwanja wa Meja Jenerali Michael Isamuhyo dhidi ya JKT Tanzania na kuibuka na ushindi wa mabao 6-0