Awali mchezo huo ulikuwa umepangwa kuchezwa katika Uwanja wa KMC Complex, Oktoba 29 lakini basi lililokuwa limebeba wachezaji wa JKT lilipata ajali wakati wakirejea kutoka Dodoma hali iliyofanya mchezo kuahirishwa.
Baada ya taarifa hiyo rasmi kutoka Bodi ya Ligi ni kwamba baada ya mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar ugenini Disemba, 21 tutarejea Dar es Salaam kucheza na JKT.