Simba Sports Club
News

Mchezo dhidi ya Dodoma kupigwa Machi 14

4 Mar 2025

Mchezo huo ulipangwa kufanyika Februari 15 lakini wapinzani wetu Dodoma walipata ajali wakiwa njiani kutoka Ruangwa, Lindi ikabidi TPLB iahirishe mchezo.

Katika ajali hiyo baadhi ya wachezaji pamoja na Maafisa wa timu walipata majeraha hivyo hawakuwa tayari kucheza mechi kwa kipindi kile.

Advertisement

Baada ya mipangilio yote kukaa sawa sasa ni rasmi mchezo huo utapigwa Machi 14 saa 10 jioni katika Uwanja wa KMC Complex.

Back to homepage
Share this story