Simba Sports Club
News

Mchezo dhidi ya De Agosto kupigwa Oktoba 9, Angola

22 Sep 2022

Uwanja wa Novemba 11 ni miongoni mwa viwanja vikubwa nchini Angola na una uwezo wa kuingiza mashabiki 50,000.

Mchezo wetu wa marudiano utapigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam Oktoba 16.

Advertisement

Kama kawaida malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda mechi zote mbili ili kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Tumetinga hatua hii baada ya kuitoa Nyasa Big Bullets kutoka Malawi kwa jumla ya mabao 4-0 kwenye michezo yote miwili tuliyocheza nao.

Back to homepage
Share this story