Simba Sports Club
News

Mchezo dhidi ya Al Masry kupigwa Benjamin Mkapa

26 Mar 2025

Ahmed amewatoa hofu Wanasimba kutokana na Uwanja wa Benjamin Mkapa kufungiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa ajili ya kupisha maboresho lakini kwa sasa ni zaidi ya asilimia 100 mtanange huo utapigwa kwenye dimba hilo.

Ahmed amesema majibu ya maboresho ya uwanja huo bado hayajatolewa rasmi na CAF lakini kwa mujibu wa maafisa kutoka Shirikisho hilo ambao wiki iliyopita walikuja kuukagua wamesema sehemu kubwa imefanyiwa marekebisho na hadi kufikia siku ya mchezo yatakuwa yamekamilika.

"Niwatoe hofu Wanasimba kuwa mchezo wetu dhidi ya Al Masry utapigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa na maandalizi yetu yanafanyika huku tukiwa tunajua mechi itapigwa kwa Mkapa," amesema Ahmed.

Ahmed ameongeza kuwa kutokana na ukubwa na umuhimu wa mchezo huo tayari viingilio vimetangazwa na tiketi zimeanza kuuzwa.

Viingilio vya mchezo huo ni kama ifuatavyo:

VIP A Sh.40,000

Advertisement

VIP B Sh.30,000

VIP C Sh.15,000

Machungwa 10,000

Mzunguko Sh.5000

Platinumz Sh.150,000

Tanzanite Sh.250,000

Back to homepage
Share this story