Simba Sports Club
News

Mazoezi ya mwisho Uwanja wa Maisara

7 Jan 2026

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na hakuna aliyepata maumivu yatakayo mfanya kuukosa mchezo wa kesho.

Morali za wachezaji zipo juu na kila mmoja ameonyesha jitihada kubwa mazoezini ili kulishawishi benchi la ufundi kumpa nafasi ya kucheza katika mchezo wa kesho.

Advertisement

Mshambuliaji Steven Mukwala aliyekuwa katika michuano ya AFCON nchini Morocco nae amejiunga na wenzake na ameshiriki mazoezi hayo.

Back to homepage
Share this story