Nyota wawili mlinda mlango, Moussa Camara na mlinzi wa kati, Abdulazak Hamza ndio pekee ambao hawajashiriki mazoezi hayo kutokana nakuwa majeruhi.
Wachezaji wengine wote wameshiriki mazoezi hayo na wapo tayari kwa mchezo ambao tunategemea utakuwa mgumu.
Advertisement
Morali za wachezaji zipo juu na kila mmoja ameonyesha jitihada kubwa mazoezini ili kulishawishi benchi la ufundi kumpa nafasi katika mchezo wa kesho.
Tutaingia uwanjani kwa kuiheshimu Petro De Luanda lakini malengo yetu ni kupambana mpaka mwisho kupata pointi tatu.