Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho kujiandaa na mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Yanga utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 11 jioni.
Katika mazoezi hayo wachezaji wameonesha kuwa tayari kwa mchezo na kutaka kupambania nembo ya klabu.
Advertisement
Kila mchezaji anajua umuhimu wa mchezo wa kesho ambapo ukiachilia mbali kuwa ni Derby lakini iwapo tutashinda tutakaa kileleni mwa msimamo kitu ambacho tunakihitaji.
Wachezaji wote waliofanya mazoezi wako vizuri na hakuna aliyepata jeraha lolote kwa hiyo Mwalimu Pablo Franco atakuwa na wigo mpana wa kupanga kikosi chake.