Simba Sports Club
News

Mazoezi ya mwisho kabla kuivaa Red Arrows

4 Dec 2021

Kikosi kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Heroes ambao utatumika kwenye mchezo wetu wa kesho wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows.

Mazoezi yameanza saa tisa alasiri ambao utakuwa muda wa mchezo wa kesho ambapo kwa nyumbani itakuwa saa 10 jioni.

Advertisement

Wachezaji wote 25 tuliosafiri nao wapo kwenye hali nzuri morali ipo juu na kila mmoja anajitahidi kufanya vizuri mazoezini ili kulishawishi benchi la ufundi kumpa nafasi kesho.

Lengo letu ni kuhakikisha tunashinda katika mchezo wa kesho ili kutinga hatua ya makundi ya michuano hii kwa kishindo.

Back to homepage
Share this story