Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na wapo kwenye hali nzuri tayari kupigania pointi tatu.
Morali za wachezaji zipo juu na kila mmoja ameonyesha jitihada kubwa mazoezini ili kulishawishi benchi la ufundi kuwapa nafasi kwenye mchezo wa kesho.
Advertisement
Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu na tunaiheshimu Tabora lakini tumejipanga kuhakikisha tunaondoka na alama zote tatu.