Simba Sports Club
News

Matola: Tupo tayari kwa Azam FC Kesho

8 Feb 2024

Matola amesema kikosi kimewasili salama jana usiku kutoka Tabora na wachezaji wapo kwenye hali nzuri kwa ajili ya kuipigania timu.

Matola ameongeza kuwa utakuwa mchezo mgumu kwakuwa ni 'Derby' na unahusisha timu ambazo zinapigania ubingwa lakini hata hivyo tumejipanga kuwakabili.

"Mara zote tunapokutana na Azam haiwezi kuwa mechi nyepesi, Azam ni timu kubwa na ina kikosi bora kwahiyo tunategemea kupata upinzani mkubwa ingawa tumejipanga kushinda," amesema Matola.

Advertisement

Kwa upande wake nahodha msaidizi, Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' amesema wao kama wachezaji wapo kamili na kila atayepata nafasi ya kucheza atakuwa tayari kuipigania timu.

"Morali za wachezaji zipo juu, tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Azam lakini tupo tayari kupambana na mwisho wa siku tupate pointi tatu," amesema Zimbwe Jr.

Back to homepage
Share this story