Simba Sports Club
News

Matola: Tunataka kumaliza ligi kwa heshima

11 Jun 2022

Matola amesema tunahitaji kushinda mechi zote tano zilizobaki kwa ajili ya kuweka heshima na kuwapa furaha mashabiki.

Matola amesema maandalizi kuelekea mchezo wetu dhidi ya Mbeya City yanaendelea vizuri baada ya wachezaji waliokuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa wamerejea na wamefanya mazoezi na wenzao.

Advertisement

Matola ameongeza kuwa wachezaji Medie Kagere na Peter Banda ndiyo pekee ambao hawajarudi lakini wanataraji kutua nchini muda wowote kuanzia sasa.

"Hatuna nafasi ya kutetea ubingwa lakini tunataka kuweka heshima kwa kushinda mechi zote tano zilizobaki ili kuwapa furaha mashabiki wetu," amesema Matola.

Back to homepage
Share this story