Matola ameyasema hayo wakati wa akiongea na Waandishi wa Habari kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo saa moja usiku.
Matola amesema tunatarajia kupata upinzani mkubwa kutoka kwa City hasa ukizingatia wametoka kufanya mabadiliko katika benchi lao la ufundi lakini tumejipanga na tupo tayari kuwakabili.
Matola ameongeza kuwa wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na jana walifanya mazoezi ya utimamu wa mwili na leo watafanya mazoezi ya mwisho tayari mchezo huo.
"Kwa upande wetu tupo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho, tunafahamu itakuwa mechi ngumu kwakuwa timu zote zimejipanga ila tutapambana hadi mwisho ili tupate ushindi," amesema Matola.
Nae mlinzi wa kulia, David Kameta 'Duchu' amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na wapo tayari kwa ajili ya kupambania alama tatu nyumbani.
"Sisi wachezaji tupo tayari kufuata maelekezo tutakayopewa na benchi letu la ufundi lengo likiwa ni kuhakikisha alama tatu za nyumbani zinapatikana," amesema Duchu.