Simba Sports Club
News Videos

Matola: Tuliwatazama Stade Malien mechi ya kwanza

29 Nov 2025

Matola amesema Stade Malien ni timu imara hasa wanapokuwa nyumbani lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda ingawa tunafahamu itakuwa mechi ngumu.

Matola ameongeza kuwa tunahitaji kupata matokeo chanya kwenye mchezo wa kesho hasa baada ya kupoteza nyumbani mechi ya mkondo wa kwanza.

“Ni mechi ngumu na zaidi sababu tunacheza ugenini, tuliangalia mechi yao ya kwanza ni timu nzuri lakini tumejiandaa kufanya vizuri na tunaamini tutaondoka na ushindi.

Advertisement

"Tunajua umuhimu wa kupata alama tatu kwenye mchezo wa kesho kwakuwa tulipoteza mechi ya kwanza hivyo kwetu ni kufa au kupona,” amesema Kocha Matola.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji kiungo mkabaji, Allasane Kante amesema maandalizi ya mchezo yamekamilika na kila mmoja yupo tayari kuipigania timu kupata matokeo chanya.

“Tumekuja hapa Mali kucheza tukiamini tutafanya vizuri, tumekuja tukijua umuhimu wa mchezo huu sababu tulishapoteza katika mchezo uliopita hivyo tumejiandaa kupata matokeo mazuri,” amesema Kanté.

Back to homepage
Share this story