Simba Sports Club
News

Matola: Tulistahili kushinda

20 Jun 2022

Matola amesema tulicheza vizuri muda wote na wachezaji walijitahidi kufuata maelekezo aliyowapa.

Matola ameongeza kuwa kipindi cha kwanza KMC waliingia kwa njia ya kuzuia hivyo wote wakawa nyuma ya mpira lakini kipindi cha pili walivyofunguka tukaweza kuwafunga.

Advertisement

"Ukiangalia mchezo mzima sisi tulikuwa bora zaidi yao, tulitengeneza nafasi nyingi na tulistahili kupata ushindi kwa kuwa tulicheza vizuri.

"KMC walitusumbua kipindi cha kwanza kwa kuwa wote walikuwa nyuma walikuwa wanazuia tu lakini tulivyorudi cha pili tulitafuta njia za kuwafungua na kufanikiwa kupata mabao yote matatu," amesema Matola.

Back to homepage
Share this story