Simba Sports Club
News

Matola: Hatutaichukulia poa Geita

30 Nov 2021

Kuelekea mchezo wetu wa kesho dhidi ya Geita Gold, Kocha Msaidizi Seleman Matola amesema hatutawadharau wapinzani hao badala yake tutaingia uwanjani kamili kutafuta alama tatu muhimu.

Matola amesema Geita si timu mbaya inacheza kitimu na tumechukua tahadhari zote kabla ya kushuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kesho kuwakabili.

Advertisement

Matola amesema kitu kizuri ni kwamba wachezaji wote wapo kambini tayari kwa mchezo huo hivyo benchi la ufundi litaamua nani aanze.

"Geita si timu mbaya, iko vizuri na tunaiheshimu. Tutaingia katika mchezo wa kesho tukiwa na tahadhari zote tunahitaji kupata alama zote tatu. Wachezaji wote wapo kambini tayari kwa mchezo wa kesho," amesema Matola.

Back to homepage
Share this story