Kocha msaidizi, Seleman Matola, amesema katika mchezo wa jana dhidi ya Coastal Union washambuliaji wetu walikosa umakini wa kutumia nafasi tulizopata.
Matola amesema kama Nahodha John Bocco na Kibu Denis wangeongeza umakini kidogo tungeweza kupata mabao lakini ndiyo mpira na tunarudi kwenye uwanja wa mazoezi kufanyia kazi mapungufu.
Mbali na hilo Matola ameongeza kuwa timu nyingi zinapokutana nasi zinacheza kwa nguvu kubwa kama fainali na kusababisha wachezaji wetu kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo.
"Kilichotokea ni sehemu ya mpira, tumepata alama moja tunarudi kujipanga kwa ajili ya mchezo ujao, nakubali tulikosa umakini katika kumalizia nafasi tulizotengeneza.
"Ukiangalia katika mechi zetu wapinzani wanatumia nguvu nyingi na kuwaumiza wachezaji wetu ndiyo maana kadi nyekundu zinatoka," amesema Matola.