Kocha msaidizi Seleman Matola, amesema katika mchezo wa leo dhidi ya Biashara United tulikosa bahati ya kufunga tu lakini tulicheza vizuri.
Matola amesema tulichokosa leo ni bahati tu ndiyo maana hata penati tuliyopata dakika za mwisho tulipoteza.
Matola ameongeza hata uwanja haukuwa rafiki ndiyo maana tumebadili mfumo na kucheza mipira mirefu ya juu ambapo kwa kiasi fulani kumetufanya kukosa matokeo.
Advertisement
"Kilichotokea ni sehemu ya mpira, tumecheza vizuri na wachezaji wamepambana lakini hatukuwa na bahati. Tumepata penati dakika mwisho pia tumepoteza.
"Mechi ya Biashara imeisha tunajipanga na mchezo unaofuata dhidi ya Dodoma Jiji," amesema Matola.