Simba Sports Club
News Videos

Matola: Bado hatujamaliza kazi

25 Oct 2025

Matola amesema pamoja na kuwa mbele kwa idadi kubwa ya mabao huku tukicheza nyumbani lakini hatutabweteka na tutaingia uwanjani kesho kwa kutafuta mabao mengi zaidi.

Aidha Matola ameenda mbali zaidi kwa kusema malengo yetu ni kupata ushindi mnono nyumbani bila kuruhusu bao.

"Tuna uzoefu mkubwa wa michuano hii, tumewahi kuwa kwenye hali kama hii lakini sasa tumejidhatiti vizuri. Ni kweli tunaongoza kwa mabao matatu lakini bado hatujafuzu."

"Malengo yetu ni kushinda kwa idadi kubwa ya mabao tena bila kuruhusu bao, tunajua haitakuwa rahisi lakini tumejipanga," amesema Matola.

Advertisement

Kwa upande wake nahodha wa timu, Shomari Kapombe amesema wachezaji wapo tayari kuhakikisha ushindi unapatikana huku akiwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi.

Kapombe amesema itakuwa mechi ngumu kwakuwa Nsingizini watakuja kwa kasi huku wakijua hawana cha kupoteza lakini tumejipanga kuwakabili.

"Haitakuwa mechi rahisi, wapinzani wetu ni timu nzuri na tunategemea watakuja kivingine hasa ukiangalia matokeo ya mchezo wa kwanza yalivyokuwa lakini sisi tupo tayari kuwakabili," amesema Kapombe.

Back to homepage
Share this story