Mashindano hayo yamendaliwa na Taasisi ya Gateway Tours & Sports inayojihusisha na kuandaa mashindano ya mpira wa miguu na matukio mbalimbali ya kimichezo.
Katika mashindano hayo Taasisi hiyo imealika makocha na maskauti kutoka maeneo mbalimbali duniani akiwemo Matola.
Advertisement
Taasisi Gateway Tours & Sports italipia waalikwa wote gharama za tiketi, malazi na Chakula kwa muda wote wa mashindano.
Mashindano haya yataambatana na mafunzo ya kutambua na kuendeleza vipaji kwa wachezaji vijana.