Simba Sports Club
News Videos

Matola afunguka maandalizi mchezo dhidi ya Azam

6 Dec 2025

Matola amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo huo ambao tunatarajia utakuwa mgumu.

Aidha Matola ameongeza benchi la ufundi pamoja na wachezaji wanafahamu ugumu wa mchezo huo kutokana na ubora wa Azam pamoja na kocha wao.

"Kwa ujumla kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho, tumejiandaa kimwili na kiakili kupambana dhidi ya Azam na malengo yetu ni kupata alama tatu."

Advertisement

"Tunafahamu haitakuwa mechi rahisi Azam wana timu nzuri wakiwa na kocha bora lakini tumejipanga na tupo tayari kuwakabili," amesema kocha, Matola.

Kwa upande wake nahodha wa timu, Shomari Kapombe amesema licha ya ubora walionao Azam lakini tupo kuhakikisha tunapambana mpaka mwisho ili kuhakikisha tunapata ushindi.

"Wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na morali ipo juu, sote tunafahamu Azam ni timu nzuri lakini tumejipanga na tupo tayari kuwakabili na kupata alama tatu muhimu nyumbani," amesema Kapombe.

Back to homepage
Share this story