Simba Sports Club
News

Matola aelezea sababu ya kushangilia bao la Ahoua

23 Dec 2024

Matola amesema tulikuwa hatupati matokeo ya ushindi kwenye uwanja huo hivyo alivyoona tumepata bao la pili alijua tupo kwenye nafasi kubwa ya kuondoka na alama zote tatu.

"Historia ilikuwa inatuhukumu, katika Uwanja wa Kaitaba tulikuwa hatupati matokeo mazuri lakini nilivyoona tumepata bao la pili ambalo lilifungwa na Ahoua nilishangilia sana nilifahamu tupo karibu na pointi tatu," amesema Matola.

Advertisement

Ahoua alifunga bao hilo dakika ya 44 kwa mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja baada ya yeye mwenyewe kufanyiwa madhambi nje ya 18 na mlinzi Abdallah Mfuko.

Katika mchezo huo mabao mengine yalifungwa na Shomari Kapombe, Fabrice Ngoma na Steven Mukwala aliyefunga mawili.

Back to homepage
Share this story