Mlinzi wa kati Henock Inonga amefunguka kuwa anafurahia kuona mashabiki wakijitokeza kwa wingi kuwalaki kila mahali wanapofika hali inayowafanya kujituma uwanjani.
Inonga ameyasema hayo baada ya kuwasili mkoani Mtwara na kushuhudia mapokezi makubwa tuliyopata kutoka kwa mashabiki wetu.
Inonga ameongeza kuwa wanachofanya mashabiki kinawafanya wachezaji kujiona wana deni kubwa na kuwa tutapambana mpaka mwisho ili kuona tunapata nini.
Advertisement
"Mashabiki wetu wanaonyesha mapenzi makubwa kwetu, hii inatuongezea morali hata tukiwa uwanjani kujituma kuhakikisha tunawapa furaha.
"Bado hatujakata tamaa na ubingwa tutaendelea kupambana hadi mechi yetu ya mwisho. Tunajua haitakuwa kazi rahisi lakini hakuna kinachoshindikana," amesema Inonga.